518079-background-hd

MWENYEKITI SEGU AONYESHA HALI YA SINTOFAHAMU.

Mwenyekiti wa kijiji cha Segu kata ya Nala Manispaa ya Dodoma Bw.Henly Malugu ameonyesha hali ya sintofahamu mara baada ya kuhojiwa na Mpita Njia juu ya uuzaji wa eneo{ardhi} katika kijiji chake jambo ambalo limepelekea wnanchi hao kukosa eneo la kupitishia mifugo yao kuelekea kwenye chanzo cha kunyweshea maji.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya wananchi hao kuzungumza na Mpita Njia  kwa masharti ya kutokutajwa majina yaoambapo walieleza kuwa mwenyekiti huyo ameuza eneo hilo na hivyo kuziba njia ya kupiyishia mifugo yao pindi wanapohitaji kwenda kunywa maji.

Awali akiongea na Mpita Njia Mwenyekiti wa mtaa huo yeye amesema kuwa hana taarifa za kuuzwa kwa eneo hilo na kuahidi kukaa na diwani kwa ajili ya kulifatilia suala hilo

Haya hivyo alipotafutwa kwa mara nyingine kwa ajili ya kuelezea hatua aliyofikia Mwenyekiti huyo aliendelea kuonyesha hali ya sintofahamu na kusema kuwa wanaendelea kushughulikia suala hilo.

**********************************************************************************************************

Kwa mujibu wa sheria inaeleza kuwa Mwenyekiti wa mtaa ndiye mwenye dhamana ya uhakiki wa ardhi katika mtaa wake. Je kwa Mwenyekiti huyu kutokuwa na majibu sahihi juu ya mgawanyo wa ardhi ni kutokujuwa wajibu wake au kuna vitu vilivyo jificha ndani yake?

Acha maoni yako hapa.

518079-background-hd

MAUAJI YA WATAFITI IRINGA –MVUMI YAMKERA RC DODOMA.

Serikali ya Mkoa wa Dodoma imelaani vikali kitendo kilichofanywa na baadhi ya wananchi wa kijiji  cha Iringa Mvumi wilayani Chamwino mkoani humo cha kuwaua kwa kuwachoma moto watafifi wawili pamoja na dereva mmoja na kuwa jeshi la polisi litahakikisha linawakamata wahusika wote.

Akiongea na Mpita Njia Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa  ambaye pia ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordani Rugimbana yeye amesema kuwa kitendo hicho ni cha kikatili mno na amewahakikishia watanzania kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwasaka wote waliohusika na mauaji hayo.

Aidha Mhe. Rugimbana amewaondoa hofu wageni wote wanaoingia mkoani Dodoma kuwa wasiwe na shaka lolote kwani kitendo hicho hakitojirudia.

Hata hivyo amewataka wananchi kutojichukulia sheria mikononi na kuondokana na imani za kishirikina pia wajijengee utaratibu wa kutoa ytaarifa katika vituo vya polisi pale wanapokuwa na mashaka na watu wasio wafahamu.Mkuu wa Mkoa Mhe. John Rugimbana

Watafiti hao wawili pamoja na dereva mmoja walitoka katika kituo cha utafiti wa kilimo cha selian jijini Arusha

Hata hivyo serikali kupitia vyombo mbalimbali vimekuwa vikitoa elimu kwa wananchi ya kutojichukulia sheria mikononi. Je kuendelea kwa vitendo hivi kunaashiria elimu hiyo kutokufika kwa wahusika?

Acha maoni yako hapa.